Mwenyekiti wa ngome ya vijana wa Chama Cha ACT – Wazalendo, Abdul Nondo ametangaza nia ya kugombea ubunge Jimbo la Kigoma Mjini akilenga kuongeza na kuchochea shughuli za kimaendeleo na mzunguko wa fedha kwenye jimbo hilo.

Nondo ametangaza nia ya kugombea nafasi hiyo katika jimbo ambalo kabla ya Bunge kuvunjwa, lilikuwa likiongozwa na kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe.

Ametoa tangazo hilo leo Julai 5, 2020,  na kusema kuwa endapo vikao vya chama chake vitampa ridhaa ya kupeperusha bendera ya kugombea Ubunge, basi atahakikisha anatekeleza na kuyaendeleza yale yote aliyoyaanzisha Mbunge mstaafu wa jimbo hilo Zitto Kabwe.

“Inawezekana mimi nikachaguliwa na Zitto akaachwa kwa sababu chama chetu kinaongozwa kwa mfumo wa demokrasia ya wazi, kwahiyo wajumbe wanaweza wakaamua kwa sababu chama chetu hakina Papa, kinasema wote ni sawa haijalishi wewe ni nani, Wajumbe wanaweza wakaamua kunichagua mimi, au wakaamua kumchagua Zitto halafu mimi wakaniambia nisubiri” amesema Nondo.

IGP Sirro ahimiza usajili kampuni binafsi za ulinzi kwenye PSGP, aeleza faida
Mgumba abainisha mafanikio kwenye jimbo lake