Watu wenye silaha wamewateka nyara abiria 36 katika barabara kuu kati ya Buea na Kumba, kusini Magharibi mwa Cameraoon katika eneo ambalo wakazi wake wanazungumza lugha ya Kiingereza.

Watekaji hao walisimamisha mabasi mawili yaliyokuwa yametoka Kumba kwenda Buea walipofika kijiji cha Ediki ambapo abiria wote waliamriwa kukabidhi vitambulisho vyao na kupelekwa mstuni sehemu isiyojulikana.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na uasi katika eneo la watu wanaozungumza Kiingereza nchini Cameroon, na lawama zimekuwa zikielekezwa kwa Serikali ya Rais Paul Biya wa nchi hiyo ambayo lugha yake rasmi ya Taifa ni Kifaransa.

Aidha, viongozi katika eneo hilo wamesema kuwa usafiri kwenye barabara hiyo umesitishwa na kazi ya kuwatafuta mateka imeshaanza.

Hata hivyo, katika nchi ya Cameroon idadi ya wanao zungumza Kiingereza ni takribani asilimia 20 ya wakazi wote  wa nchi hiyo ambao ni milioni 20.

Mfahamu Joseph Bombardier mwanzilishi wa kampuni ya Bombardier
Mwandishi aliyefichua rushwa CAF, auawa kwa kupigwa risasi