Abiria 900 waliokwama kwa siku mbili katika eneo la Pugu Mnadani, Dar es Salaam baada ya Treni waliyokuwa wakisafiri nayo ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kwenda mikoa mbalimbali kushindwa kuendelea na safari, wamelalamikia ukosefu wa huduma muhimu katika eneo.

Abiria hao wameeleza kuwa wamepata ya ukosefu wa chakula na maji kwa kipindi cha siku mbili walichokwama katika eneo hilo hali inayowatesa zaidi watoto waliokuwa katika msafara huo. Wameongeza kuwa safari hiyo ilianza kwa kusuasua na kwamba TRL haikuwapa taarifa yoyote kuhusu kuzibwa kwa reli kutokana na ajali ya treni ya mizigo.

“Nina watoto wawili mmoja bado mdogo anahitaji uji na sehemu yenyewe hakuna huduma yoyote hata kupiga uji wa mtoto ni shida,” alisema abiria mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Eliza Denis.

Hata hivyo, Meneja Uhusiano wa TRL, Midladj Mez alieleza kuwa kampuni hiyo iliwapa taarifa abiria wote kuhusu kutokea kwa ajali ya treni hiyo ya mizigo, katika eneo la Soga Mpini.

Mourinho Anusurika Na Adhabu Ya FA
Ronaldo Ni Gangwe Wa Wafalme Santiago Bernabeu