Abiria wanaotumia usafiri wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (Udart), wameulalamikia mradi huo kwa kushindwa kutatua kero za muda mrefu ikiwemo kusubiria vituoni zaidi ya dakika tano.

Aidha, wamesema kuwa imekuwa kawaida hasa asubuhi abiria kusubiri abiria kusubiri mabasi hayo zaidi ya dakika zilizowekwa na mradi huo.

Baadhi ya wakazi wa kimara wamesema kuwa mabasi hayo yamekuwa yakichelewa kufika vituoni bila hata ya abiria kupewa taarifa yoyote kuhusu kuchelewa kwa mabasi hayo.

Hata hivyo wamesema, ukiachilia mbali kero hiyo ya mabasi hayo yanayopita kila baada ya dakika tano hata kama abiria hakuna, wametoa ushauri kwa Udart kuwa na utaratibu wa kutoa mabasi mengi asbuhi na jiono kwa kiasi kikubwa  ili kupunguza msongamano wa watu vituoni.

 

 

Maombi ya dhamana ya Lema kusikilizwa leo
Makunga: Wanahabari sheria mpya isiwatishe