Takribani watu wasiopungua 70 wamefariki na wengine wamejeruhiwa baada ya treni la abiria kuwaka moto nchini Pakistan.

Imeelezwa kuwa video zilizonasa tukio hilo zimeonesha mabehewa matatu yakiwa yanawaka moto na kuteketea huku moshi mzito ukitoka kwenye madirisha na mashuhuda wamesema wamesikia vilio vya watu  wakilia na kupiga mayowe ya kuomba msaada.

Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri wa Mamlaka ya reli nchini humo, Sheikh Rahid Ahmed amesema kuwa vifo vingi vimetokea baada ya abiria kujirusha kwenye madirisha kuokoa maisha yao huku treni likiendelea kutembea.

Ahmed ameseama ajali hiyo imesababishwa na mlipuko wa jiko la gesi ambalo abiria walikuwa wanapikia kifungua kinywa asubuhi jambo ambalo ni kinyume na sheria kwa abiria kuingia na jiko la gesi kwenye treni.

Ajali hiyo imetokea kwenye treni l Tezgam Express, ambalo linafanya safari zake kwenye miji ya Karachi na Rawalpindi.

Kamishna msaidizi wa mji wa karibu Multan, Mansoor Ahmed, amethibitisha vifo vya watu 70 na 30 waliojeruhiwa huku wengine wakiwa na hali mbaya na wamekimbizwa katika hospitali ya wilaya.

Waziri mkuu wa nchi hiyo Imran Khan, ametoa taarifa kupitia ukurasa wake wa tweeter kuwa amepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali hiyo.

” Nimehuzunishwa sana na ajili mbaya ya treni la Tezgam, nawapa pole wafiwa wote na nawaombea majeruhi wapone haraka, nimeagiza uchunguzi ufanyike haraka”

Ikumbukwe kuwa mwezi Julai watu takribani 23 walifariki nchi humo baada ya kujaa kwenye mabehewa ya treni la mizigo.

Abalora wa Azam FC aitwa Black Stars, #BringBackTheLove kuwapeleka AFCON 2021
Dick Advocaat achukua nafasi ya Jaap Stam

Comments

comments