Msichana mwenye umri wa miaka 19, Parker Hogan amefunguliwa mashtaka kwa tuhuma za kumsaidia rafiki yake kujiua mwanzoni mwa mwezi huu.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyowasilishwa mahakamani, eneo la New Hampshire nchini Marekani, mtuhumiwa huyo alikuwa na marehemu Michael Buskey alipokuwa anapanga kujiua na alimsaidia njia yenye uhakika ya kujimaliza kwa bunduki.

Imeelezwa kuwa baada ya Hogan kumshawishi na kumueleza Buskey jinsi ya kujipiga risasi na kwamba alikaa mbali kidogo akisubiri hadi aliposikia mlio wa risasi na kwenda kushuhudia.

Ripoti ya polisi iliyotolewa tena na shirika la habari la ABC, Hogan alisubiri hadi siku iliyofuata ndipo alipotoa taarifa polisi kuhusu tukio hilo huku akidanganya kutofahamu chanzo chake.

Parker Hogan akiwa mahakamani

Ingawa mahakama ilikubaliana na taarifa za polisi kuwa Buskey alijiua mwenyewe, mama yake mzazi amesema kuwa anaamini kuna mengi zaidi kuhusu tukio hilo.

“Ninadhani kuna mengi nyuma ya hili. Mawazo yangu binafsi, siwezi kumzungumzia mtu mwingine. Ninaamini kila kitu kitawekwa hadharani hivi karibuni na kila mtu atafahamu kilichotokea kweli,” alisema mama huyo.

Mwendesha mashtaka amesema kuwa endapo Hogan atakutwa na hatia atakabiliwa na kifungo cha hadi miaka saba jela.

Magazeti ya Tanzania leo Juni 1, 2018
Video: Chadema hawafai kukabidhiwa dola- Dkt. Mollel

Comments

comments