Ngome ya FC Shakhtar Donetsk ya nchini Ukarine, imeendelea kubomolewa baada ya klabu ya AC Milan kukamilisha usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Brazil, Luiz Adriano de Souza da Silva.

Adriano ameondoka Shakhtar Donetsk ikiwa ni baada ya siku mbili ambapo ilishuhudia mbrazil mwingine Douglas Costa akisajiliwa na mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich.

Usajili wa Andriano, ulithibitishwa rasmi baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina ya wakala wake na viongozi wa klabu ya AC Milan yaliyochukua nafasi kwenye mgahawa wa Casa Milan, uliopo mjini Milan nchini Italia usiku wa kuamkia jana.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano ambao utamuweka San Siro hadi June 30 mwaka 2020.

Adriano, anatarajia kujiunga na wachezaji wenzake tayari kwa kuanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi na anatarajiwa kuwa mtetezi mzuri wa AC Milan katika safu ya ushambuliaji.
Akiwa na FC Shakhtar Donetsk kuanzia mwaka 2007, Adriano alicheza michezo 162 na kufunga mabao 79.

AC Milan Wakubali Dili La Kumsajili Mshambuliaji Wa Colombia
Michuano Ya Wimbledon, Nadal Atupwa Nje