Klabu ya AC Milan imemsajili mshambuliaji wa zamani wa Mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC, Mario Mandzukic kwa kumsainisha mkataba hadi mwishoni mwa mimu huu.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Croatia amejiunga na AC Milan kama mchezaji huru, baada ya kuachana na Al-Duhail ya Qatar Julai mwaka jana na mkataba wake na AC Milan una kipengele cha kuongeza muda zaidi, endapo ataonesha kwango madhubuti.

Meneja wa AC Milan Stefano Pioli, anaamini usajili wa Mandzukic utaleta uzoefu mkubwa kwenye kikosi chake, ambacho kinafukuzia taji la kwanza la ‘Serie A’ tangu mwaka 2011.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 ataongeza uzoefu zaidi katika eneo la Ushambuliaja AC Milan, ambalo linaongozwa na vijana wengi huku mkongwe akiwa mmoja tu katika Kiwango bora, Zlatan Ibrahimovic.

Kutokana na Ibrahimovic kurejea kutoka kwenye majeraha, akifunga mara mbili wakati wa kurudi katika ushindi wa Jumatatu dhidi ya Cagliari, uwepo wa Mandzukic utampa Pioli fursa ya kuwa na machaguo mengi katika kikosi chake cha kwanza.

Ingawa ilikuwa Julai 2020 wakati Mandzukic aliondoka Al-Duhail, Mcroatia huyo hakucheza michezo ya ushindani tangu Machi mwaka jana, kwa hivyo Pioli atakuwa na uamuzi wa kufanya ikiwa atamleta moja kwa moja kwenye mipango yake.

Mandzukic alishinda taji la Scudetto (Serie A) mara nne wakati wake na Juventus FC, pia alishinda Bundesliga mara mbili na Ligi ya Mabingwa wakati alipokuwa na FC Bayern Munich.

AC Milan, ambao wako alama tatu tofauti na Inter kileleni mwa Serie A, watamenyana na Atalanta kwenye ligi Siku ya Jumamosi kabla ya Milan Derby kwenye Coppa Italia Januari 26. Mandzukic anaweza kuwa kwenye kikosi cha michezo hiyo yote miwili.

Atavaa jezi namba 9 ambayo hapo awali iliwahi kuvaliwa na Wachezaji kama Filippo Inzaghi , Alexandre Pato, Mattia Destro, Andre Silva, Fernando Torres na Gonzalo Higuain.

Wachambuzi wamchukiza Manara, atuma ujumbe Cameroon
Rwanda yarejea 'lockdown' tena