Mgodi wa Uchimbaji wa Dhahabu ACACIA North Mara Uliopo Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara unatarajia kuanza kulipa malipo ya fidia ya ardhi kiasi cha shilingi billioni 3.8 ambapo zaidi ya wananchi 200 kutoka vijiji Vilivyofanyiwa tathimini mwaka 2011-2012 pamoja na awamu za 35, 41,na 42 katika vijiji vya Nyabichune, Mjini kati, Nyangoto, na Nyakunguru watalipwa fedha hizo.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Idara ya Jamii Endelevu ya Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, Richard Ojendo Mara ambapo amesema kuwa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara unakusudia kuanza zoezi la malipo ya fidia ya ardhi kwa wananchi waliopo kwenye vijiji Vinne katika eneo la Nyamongo.

Amesema kuwa vijiji hivyo vilifanyiwa tathimini katika awamu ya 20 ya mwaka 2011-2012 pamoja na awamu za 35,41,na 42 vitalipwa.

Pia amesema kuwa wananchi wa kijiji cha Nyabichune waliofanyiwa tathimini eneo la Makerero awamu ya 47 waende kuchukua malipo yao ya fidia ifikapo 04 Machi Mwaka huu.

“Zoezi hili ni kwa wananchi halisi wa maeneo na awamu ambazo zimetajwa ambao taarifa zao zilichukuliwa na mgodi kwa ajili ya malipo ya fidia na orodha kamili wananchi watakaolipwa tayari tumekabidhi viongozi wa vijiji na vitongoji husika,”amesema Ojendo.

Hata hivyo, ameongeza kuwa malipo kwa awamu nyingine yataendelea kulipwa na wahusika watajulishwa pale muda utakapofika na kuomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa dhidi yao na Mgodi wa Uchimbaji wa Dhahabu ACACIA North Mara.

AAR yatoa matibabu bure kwa washiriki Kili Marathon 2019
Wajasiliamali watakiwa kuwa wabahili

Comments

comments