Kampuni ya Acacia iliyodumu kwa miaka minne ndani ya soko la hisa Dar es salaam (DSE), imeondolewa katika orodha ya kampuni zilizopo kwenye soko la hisa kuanzia leo, Novemba 18, 2019.

Akiongea leo jijini Dar es salaam, Meneja Miradi wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE)  Emmanuel Nyalali, amesema kampuni hiyo iliorodheshwa tangu Desemba 2011 ikijulikana kama African Barrick Gold, na Novemba 2014 ilibadili jina na kuitwa Acacia.

Kampini hiyo ilianza kufutwa katika Soko la Hisa la London Uingereza (LSEG) tangu Septemba mwaka huu, hivyo utaratibu wote umefuatwa.

“Tangu Septemba 2019 Acacia ilikuwa imeshafutwa kwenye soko la Hisa la London (LSEG), ambalo ndio soko lake mama, hivyo taratibu zilikuwa zinamaliziwa tu na Ijumaa iliyopita Bodi ya DSE ilitoa maamuzi hivyo kuanzia leo kampuni hiyo inafutwa kwenye orodha ya makampuni kwenye DSE”, amesema Nyalali.

Imeelezwa kuwa kufutwa kwa kampuni hiyo kutapunguza ukubwa wa mtaji wa soko la hisa DSE kutoka sh 19.67 trilioni hadi sh 16.94 trilioni.

Heche na Mchungaji Msigwa wajisalimisha
Undani wa Picha ya mtoto akichungulia darasani na sufuria mkononi

Comments

comments