Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia imeripoti kuwa imepoteza pato lake kwa asilimia 50 katika awamu ya kwanza baada ya kupunguza operesheni zake za uchimbaji katika machimbo yake maarufu nchini Tanzania kufuatia mgogoro wa kodi baina yake na serikali.

Acacia, ambayo ni kampuni moja wapo inayoendeshwa na kampuni mama ya Canada Barrick Gold na ikiwa ndiyo kampuni kubwa ya uchimbaji imesema kuwa uzalishaji wa dhahabu ulishuka kwa asilimia 45 katika kipindi cha kwanza.

Aidha, hisa za kampuni ya Acacia zilizo orodheshwa katika soko la hisa la Uingereza ziliporomoka kwa asilimia 8.8 na sasa zimeshuka kwa zaidi ya asilimia 70 tangu serikali ya Tanzania ilipozuia usafirishaji wa malighafi inayotokana na machimbo ya dhahabu ya Bulyanhulu mwezi Machi 2017.

Hata hivyo, Serikali iliunda tume ya uchunguzi kufuatilia suala hilo na mwezi uliofuatia matokea ya uchunguzi huo yalionyesha kuwa Tanzania imekoseshwa trillion za mapato kutokana na mauzo ya madini ya mchanga unaotolewa nje na makampuni hayo.

 

UN kusimamia mdahalo wa Rwanda na Burundi
Ndugai adai Bunge haliwezi kuidhinisha fedha za matibabu ya Lissu