Mbunge wa viti maalum (CCM) Lucy Mayenga amesema kuwa Jeshi la Polisi nchini Tanzania kwa sasa linafanya kazi nzuri ambayo inaonekana na kusema kuwa kitendo wanachokifanya kuwadhibiti baadhi ya wanasiasa na viongozi ni sawa kabisa kwani wanawashikisha adabu.

Ameyasema hayo bungeni na kuwaambia viongozi wa jeshi la polisi akiwepo IGP Sirro kuwa asiwe na wasiwasi wowote kwani wanafanya mambo mazuri kwa madai kuwa wapo wabunge walizoea kutukana viongozi wa nchi na kusema maneno hovyo kwenye mikutano mbalimbali.

“Hii nchi watu walizoea kudeka, watu walikuwa wamezoea kuropoka maneno ya ajabu ajabu kila siku, watu walikuwa wamezoea kutukana kwenye mikutano hovyo hovyo lazima ifike wakati tushikishwe adabu, vyama vyote vya siasa ukiwa CCM ukiwa chama chochote lazima ifike wakati ujue kwamba nchi lazima itawalike isiwe kwamba watu wanakuwa huru kiasi mtu anaweza kuamka leo asubuhi na kufanya anachotaka kwa hiyo lazima ajue kwamba akifanya jambo lolote likiwa na adhima mbaya atashughulikiwa,”amesema Mayenga

Hata hivyo, amewapongeza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga na kusema hao ni watu ambao wanafanya kazi vizuri sana.

Mabasi ya mwendokasi yasitisha safari baadhi ya maeneo Dar
Joti afafanua juu ya ghorofa lake kubomolewa