Chama cha ACT- Wazalendo kimepanga kuzindua kampeni zake za uchaguzi Mkuu, Jumapili, Agosti 30 maeneo ya Mbagala, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Taarifa za uzinduzi wa kampeni zilitolewa na afisa habari wa chama hicho, Abdalah Khamisi ambaye alieleza kuwa chama hicho kitaanza rasmi kuwanadi mgombea urais, Anna Mghwira na mgombea mwenza Hamad Musa.

Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe ambaye alikuwa mwanachama wa Chadema, anatarajiwa kuongoza kampeni hizo na kuwa kivutio zaidi kutokana na historia yake nzuri ya kuvumbua ufisadi pamoja na msimamo wake wa kuwatetea wananchi bungeni.

Mgombea urais wa ACT- Wazalendo, Bi. Anna Mghwira aliteuliwa na chama hicho baada ya mmoja kati ya waasisi wa chama hicho, Profesa Kitila Mkumbo kukataa kugombea nafasi hiyo licha ya kuchukuliwa fomu katika ofisi za Tume ya Taifa.

Chama hicho kitakuwa chama cha tatu kuzindua rasmi kampeni zake baada ya CCM iliyozindua Jumapili iliyopita na Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa wanaopanga kufanya uzinduzi Jumamoji ijayo.

Hodgson Apata Kigugumizi Cha Kutaja Kikosi
Stars Yaanza kuivutia Kasi Nigeria