Chama cha ACT- Wazalendo kimesema kuwa tangu kiingie kwenye matatizo na jeshi la polisi siku za hivi karibuni kumeathiri sehemu kubwa ushiriki wao katika kampeni za marudio ya uchaguzi wa madiwani.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, ambapo amesema kuwa kama jeshi la polisi litataka kuwahoji viongozi wa chama chao basi litapaswa kutengeneza utaratibu ambao hauathiri ushiriki wao wa kampeni za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi huu.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu aliitikia wito wa jeshi la Polisi (Kituo cha Makosa ya Kifedha, Kamata, Dar es salaam) kama alivyohitajika kwenda kutoa maelezo ya ziada kuhusu nyaraka na vifaa vya kieletroniki vilivyochukuliwa kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Chama

“Kama tulivyoeleza huko awali, danadana hizi za Jeshi la polisi zimeathiri kwa sehemu kubwa ushiriki wetu kwenye Kampeni za marudio ya uchaguzi wa madiwani. Kama jeshi la polisi litataka kuwahoji viongozi wetu litapaswa kutengeneza utaratibu ambao hauathiri ushiriki wetu wa Kampeni,”amesema Shaibu

Amesema kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Chama, Yeremia Kulwa Maganja anatarajiwa kufanya ziara kwenye mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara kushiriki ufunguzi wa Kampeni kwenye kata zilizopo kwenye mikoa hiyo ambazo zinarudia uchaguzi.

 

Kenya kuwalipa wafugaji waliotaifishwa Ng'ombe Tanzania
Magazeti ya Tanzania leo Novemba 10, 2017