Chama cha ACT Wazalendo nchini kimetaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya Rais wa Marekani, Donald Trump kufuatia hatua yake ya kutoa matamshi ya chuki dhidi ya mataifa ya Afrika na raia wanaotoka bara la Afrika.

Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Kamati ya masuala ya mambo ya nje ya chama hicho, Venance Msebo katika taarifa iliotolewa na chama hicho.

”Kwa niaba ya chama, ninashutumu pakubwa matamshi ya ubaguzi wa rangi ya rais Donad Trump.Kuwaita Waafrika na watu kutoka Afrika wachafu ni ubaguzi wa rangi na tabia ya chuki ya utawala mpya wa Marekani kwa bara Afrika na ulimwengu hautanyamaza’,’amesema Msebo

Amesema kuwa wanapongeza hatua ya taifa la Botswana kuhusu suala hilo na wanajivunia taifa hilo kuwa limekuwa katika mstari wa mbele kushutumu kwa vitendo hivyo kuhusu watu wa Afrika.

Hata hivyo, ameyataka mataifa ya bara Afrika kutathmini matamshi hayo ya rais wa Marekani kama muamko kwa mataifa ya Afrika ili kujiimarisha kiuchumi na kukabiliana na umasikini kwa lengo la kujisimamia.

Mgogoro wa shamba wasababisha vifo
DC Hapi ampa mwezi mmoja mkandarasi kukamilisha mradi

Comments

comments