Chama cha ACT-Wazalendo, kimesema ujumbe wa kwaresma mwaka 2018 uliotolewa na Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania (TEC) kuhusu masuala ya kisiasa, Kiuchumi na kijamii unaonyesha jinsi demokrasia inavyominywa nchini.

TEC imetoa ujumbe huo Februari 2018 ulioandikwa na maaskofu wote 35 wa baraza hilo, wakiongozwa na Rais wake, Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa upo katika kitabu cha kurasa 20 ikiwa ni maandalizi ya ibada ya siku 40, kipindi ambacho ni cha mfungo wa kukumbuka siku 40 za kristo kufunga na kwenda jangwani.

Akizungumza na wanahabari leo Februari 12, 2018 katibu wa itikadi na Uenezi na Mawasiliano wa chama hicho, Ado Shaibu amesema.

”Tunawapongeza sana viongozi wetu kwa kujitokeza waziwazi kuonyesha ugandamizaji wa haki unaoendelea nchini.”

”TEC kutoa waraka wa kiuchungaji ni kurasa mpya katika siasa zetu tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 umalizike” amesema Ado Shaibu.

Katika ujumbe huo, TEC wamezungumzia hali ya kisiasa na kusema uamuzi wa serikali kuzuia, maandamano , mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni kwenda kinyume cha katiba ya nchi.
Shaibu ameitaka Serikali kuondoa zuio batili la vyama vya siasa kutofanya mikutano ya hadhara ya kuzungumza na wananchi.

Mbali na hilo, Shaibu ameiomba Serikali itoe taarifa ya uchunguzi kupotea kwa mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Azory Gwanda aliyefikisha siku 84 tangu kupotea kwake sanjari na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kibondo, Simon Kanguye.

Video: Lowassa amenifundisha mengi- Bashe
Edo Kumwembe ampa ufalme John Bocco