Mwanaume mmoja aliyetajwa kwa jina la Mohammad Tariq Mahmood, mkazi wa jiji la London nchini Uingereza amedai kuzuiwa kupanda ndege yeye na familia yake kwa sababu tu ni Muislam.

Mahmood ameiambia CNN kuwa yeye na wanae walikuwa wanataka kusafiri  kwenda Los Angeles nchini Marekani kufanya matembezi na kwamba tayari walikuwa wamekata tiketi na mizigo yao ilikuwa imetangulia ndani ya ndege lakini walijikuta wakikataliwa kupanda ndege na kuondolewa katika uwanja huo wa ndege bila sababu za msingi.

Mwanaume huyo alieleza kuwa katika safari hiyo alikuwa anaongozana na wanae wawili pamoja na kaka yake na shemeji yake lakini maafisa wa uwanja wa ndege walimuita na kumueleza kuwa hawataweza kusafiri wote na kwamba huenda wachache kati yao ndio watakaoruhusiwa kusafiri. Hata hivyo anasema hakuelezwa nani kati yao angeweza kuruhusiwa.

“Familia yangu ilikuwa na majonzi makubwa na walianza kububujikwa na machozi,” alisema Mahmood.

Hata hivyo, Uongozi wa uwanja wa ndege ulipoulizwa ulidai kuwa suala la dini haliwezi kuwa sababu ya kumzuia mtu yeyote kusafiri.

Msemaji wa idara ya Uhamiaji na ulinzi wa mipaka wa Marekani, Jim Burns aliiambia CCN kuwa kigezo cha dini hakiwezi kumzuia mtu kusafiri au kuvuka mpaka. Alisema kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria ya Uhamiaji na haki za binadamu.

Mahmood amesema kuwa bado hajapangua mizigo yake kwa kuwa anaamini safari yake itakubaliwa siku za hivi karibuni kwani anaamini kuwa hakutendewa haki.

 

Ben Pol Amuomba Radhi Ali Kiba
50 Cent Amburuza Rick Ross Mahakamani