Jeshi la Polisi katika Kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya linamshikilia mwanaume mmoja kwa tuhuma za kushiriki kumbaka, kumuua na kisha kumtundika kwenye nyaya za nguzo za umeme mpenzi wake.

Akizungumzia tukio hilo, mkuu wa Polisi wa Jimbo la Mwea Magharibi, Joseph Matiku amemtaja marehemu kwa jina la Damaris Njeri mwenye umri wa miaka 22.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Polisi, Damaris alibakwa na kuuawa kisha kutundikwa juu ya nyaya za umeme katika kijiji cha Rukanga, Alhamisi iliyopita. Alisema kuwa aliuawa katika eneo tofauti na kutundikwa kwenye nyaya hizo katika eneo lingine.

Baba wa marehemu, aliyetajwa kwa jina la Muriuki Kagunda aliiambia Citizen kuwa alipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kupokea simu kutoka polisi akielezwa kuwa binti yake ameuawa.

Chanzo cha karibu na familia hiyo kimeeleza kuwa mpenzi wake anayetuhumiwa kuwa mhusika alimpigia simu baba yake marehemu akimlalamikia kuwa mwanaye anamsaliti (anachepuka).

Matiku amesema kuwa wanaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo na atapelekwa mahakamani upelelezi ukikamilika na kujirisha kuwa ana kesi ya kujibu.

Mwanjelwa ang'aka, 'Nataka uache kiburi'
B12 afunguka kinachokosekana sasa kwenye Hip-Hop, Rap Bongo

Comments

comments