Riziki  ya kuku miguuni mwake ndiyo  msemo ambao Wanafunzi wa chuo  cha Dar es Salaam School of journalism  kilichopo jijini Dar es salaam wanaweza kuusema pindi wanapozungumzia   zawadi zilizotolewa leo na kitengo cha ADALIPA kilichopo chini ya kampuni ya  data vision international.

Meneja masoko wa ADALIPA Bw. Maclean Mwaijonga amethibitisha usemi huu baada ya kugawa simu aina ya Samsung tablet na tishet kwa baadhi ya wanafunzi kupitia kampeni ya ‘Foleni sasa basi’ ambao ni watumiaji wa huduma za adalipa kwa lengo la kuendelea kuwahamasisha wanafunzi wanaofanya malipo kupitia huduma hiyo.

IMG_1374

Akitoa ufafanuzi juu ya zawadi hizo Bw. Maclean amesema kuwa utolewaji wa zawadi hiyo umezingatia vigezo vya ulipaji ambapo mshindi wa simu Bw. Michael Charles ndiye anaetumia huduma ya ada lipa mara nyingi zaidi chuoni hapo.

Akiwa chuoni hapo Bw. Maclean amewashauri wanafunzi hao kuendelea kutumia huduma ya adalipa ambayo ni rahisi na haraka ambapo mtumiaji anaweza kufanya malipo muda wowote na kwa usalama zaidi.

Hata hivyo amewasihi wanafunzi kuendelea kutumia huduma ya adalipa  ili kuendelea kujipatia zawadi mbalimbali zitolewazo na kampuni yake.

Hata hivyo zawadi ya simu imekabidhiwa kwa muwakilishi kutoka katika chuo hiko baada ya mshindi Michael Charles kutokuwepo mazingira ya chuoni kutokana na dharura.

Video: 'FOLENI SASA BAASI' - M-Lipa
Copa America 2016 - Kaka Kuziba Pengo La Douglas Costa