Wazazi/ walezi wa wanafunzi pamoja na shule mbalimbali nchini zimefaidika na huduma ya AdaLipa inayowawezesha kutuma na kupokea malipo ya ada kwa njia ya simu.

Baadhi ya wazazi/walezi wameeleza kuwa huduma hiyo imewasaidia kuokoa muda waliokuwa wakiutumia kupanga foleni katika mabenki mbalimbali kwa ajili ya kulipia ada za wanafunzi huku wakitakiwa kuendelea na kazi zao mbalimbali.

“Kabla sijajiungana AdaLipa, nilikuwa na wakati mgumu ikifika muda wa kulipia ada, foleni kila benki… nilikuwa napata wakati mgumu kwa sababu ofisini nakuwa busy muda ambao Benki ziko wazi. Wakati mwingine nilikuwa namkwaza mwanangu kwa kuchelewesha ada,” Pendo Elisha, Mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam aliiambia Dar24 wikendi iliyopita.

“Lakini tangu nijiunge na huduma ya AdaLipa kwakweli kila malipo ya ada namalizia kwenye simu yangu kwa muda mfupi sana,” aliongeza.

Huduma ya AdaLipa sio tu kwamba inarahisha mzazi kulipia ada, bali pia humkumbusha kuhusu malipo ya ada kwa muhula na shule husika, kwa kutumia ‘Notifications’ maalum kwenye simu yake ili kumrahisishia kupanga mipango yake ya kifedha.

AdaLipa ambayo ni sehemu ya huduma salama inayoendeshwa kwa mfumo wa M-Pesa, inamuwezesha mzazi pia kufuatilia hatua mbalimbali za malipo yake ya ada kwa njia ya simu.

Net bargain-priced tailor-made essay, school assignment, basic research document, review
Video Mpya: Dogo Janja - My Life