Takriban watu 28 wameuawa usiku wa kuamkia leo kwa kukatwa mapanga na kupigwa risasi na waasi wanaodaiwa kuwa wa ADF, katika kijiji cha Makungwe, kilichopo kilomita 60 kusini mashariki mjini Beni nchini DRC.

Hadi kufikia majira ya jioni hakuna kundi lililodai kuhusika na tukio hilo, huku baadhi ya mashuhuda wakisema hali ni mbaya na wanaomba msaada kwa Serikali ya DRC ili kuweza kuwapatia ufumbuzi huku wakiomba msaada kwa waliojeruhiwa.

Eneo mojawapo ambalo limehusika na mauaji ya watu huko Beni nchini DRC. Picha ya Africanews.

Mmoja wa mashuda hao Sadame Patanguli amesema, “wengine wamechomwa moto na wengine wameuawa kwa risasi wengine wameuawa kwa mapanga na kuna watu hawajulikani walipo halafu cha kushangaza maadui hawa wanapitia kwenye kambi tu ya jeshi inashangaza.”

Hata hivyo Makamu Mkuu wa Kiongozi wa Wilaya ya Beni, Kanali Marcel Kaluni amesema anawaomba raia kuwa wangalifu kwani adui hana muda na hawezi kutambulika kirahisi na kwamba Jeshi la nchi hiyo lipo makini katika kuhakikisha wanakuwa salama na msako dhidi ya waliotenda tukio hilo unaendelea.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 24, 2023
Polisi yawapa neno wanaonyimwa unyumba, kupigwa na wake zao