Huko nchini Kenya kijiji cha Chabarus Kaunti Ndogo ya Cherang’any baba mmoja aliyefahamika kwa Fred Wekesa amemuua mwanaye David Wafula mwenye umri wa miaka 9 mara baada ya kumpa adhabu ya kichapo na kumsababishia kifo.

Hivyo mahakama ya juu ya mjini Kitale imemuhukumu baba huyo kifungo cha miaka 15 kwa kosa la kumuua mwanaye wa kiume miaka mitatu iliyopita.

Hata hivyo mashaidi mbalimbali walisema jamaa huyo ni mtumiaji wa bangi na mke wale alimtoroka kwa sababu ya ubishi na udhalimu.

Korti iliambiwa na upande wa ushahidi kuwa, Wekesa ni mtu anayependa vita kwa sababu ya uraibu wake wa bangi na amekuwa akiwatishia kuwaua wanakijiji chake.

Inadaiwa kuwa, Wekesa alitaka kuuficha ukweli kuhusu kifo cha mwanawe kwa kusema ilikuwa ajali ya barabarani wakisafiria bodaboda lakini chifu na walioshuhudia walitoa ushahidi tofauti.

uchunguzi wa daktari ulisema, mvulana huyo alivuja damu kwa ndani na ndio iliyosababisha kifo chake.

Baadaye Wafula alikiri kosa lake na kutaka korti kumsamehe.

Nilikuwa tu nikimwadhibu mtoto na ilitokea bahati mbaya. Nasikitika hasira kali ilisababisha nimpige vibaya mtoto wangu na kumuua,” aliomba.

Baada ya ushahidi ulioletwa mbele yangu hapa kortini, nakufunga kifingo cha jela miaka 15 kwa kusababisha kifo cha mtoto wako,” alisema Jaji katika mahakama ya Kitale, Hillary Chemitei wakati akiisoma hukumu hiyo.

Wazazi wake walifurahi kwani tabia yake ya kuwa mtu mbishi na dhalimu ilikuwa imewachosha, walisema kifungo cha jela kitamsaidia kurekebika na kuwa mtu mwema.

Alisson Becker kuvaa gwanda dhidi ya SSC Napoli
Jean-Pierre Bemba kuwania Urais DRC

Comments

comments