Beki wa klabu ya Sevilla CF ya nchini Hispania, Adil Rami amefichua siri iliopo kati yake na meneja wa PSG Unai Emery.

Rami amesema Emery ameweka mipango mikakati ya kutaka kumuhamisha Sevilla CF na kumpelekea na PSG, kutokana na ukaribu uliojengeka baina yao wakati meneja huyo alipokua kiongozi wa benchi la ufundi huko Ramón Sánchez Pizjuán Stadium.

Beki huyo kutoka nchini Ufaransa amesema wakati Emery akiwa Sevilla CF alimsaidia kwa kiasi kikubwa na walikua na ukaribu wa kutosha kutokana na kiwango chake cha soka ambacho kilifanikisha mipango ya meneja huyo.

“Niliwahi kuzungumza na Emery wakati wa majira ya kiangazi na aliweka dhamira ya kunihamishia PSG,” Rami alifichua siri hiyo alipohojiwa na kituo cha Redio cha Montecarlo.

“PSG walipokua kwenye mipango ya kumruhusu David Luiz ili ajiunge tena Chelsea, ndipo mazungumzo kati yangu na Emery yalianza.

“Wakati hayo yakiendelea nilikaa kimya bila kusema chochote, lakini niliamini kama jambo hilo lipo, ipo siku litatokea kwa vitendo.

“Kwa sasa ninaendelea kucheza Sevilla CF, na nipo kama msafiri ambaye wakati wowote anakua njiani tayari kwa safari.

Pep Guardiola Amfukuza Sergio Aguero Man City
Georges Leekens Abebeshwa Mikoba Ya Milovan Rajevac