Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema kuwa muswada wa sheria wa Vyama vya Siasa vipo vifungu vimetengenezwa maalumu kwa viongozi kama kina Nape Nnauye na Hussein Bashe ili kuwawekea mazingira magumu kutokana na yanayoendelea ndani ya chama chao.

Ameseyama hayo hii leo jijijni Dar es salaam wakati akifanya mahojiano na kituo kimoja cha radio, ambapo amesema kuwa katika muswada huo kipo kifungu ambacho kinamzuia mtu anayefukuzwa chama chake kuhamia chama kingine na kupewa nafasi ya kugombea.

Aidha amesema kuwa kuna fukuto kubwa linaloendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi hivyo wao kama upinzani wanahitaji kutumia udhaifu na migongano iliyopo ndani ya chama hicho kama fursa ya kujinufaisha nayo ndiyo maana wanaungana pia kupinga muswada huo wa sheria ya vyama vya siasa.

”Niweke wazi kwamba watu kama kina Nape, Bashe ndiyo wanaowekewa vifungo vya namna hii. Sisi wapinzani tunachukua fursa wao wanavuruga basi na sisi lazima tuwavuruge. CCM kwa kuwa wanajua wanalo fukuto wanatengeneza mazingira ya kuwanyima nafasi za kugombea 2020 endapo watashugulikiwa,”amesema Shaibu

 

 

Mfahamu Rais Mteule wa DRC, Tshisekedi aliyekuwa akikataa madaraka
Serikali yazinyooshea kidole shule binafsi