Baada ya kufanikiwa kuibakisha timu ya Kagera Sugar katika ligi kuu Tanzania bara msimu ujao kocha Adolf Rishard ameapa kurejesha makali ya ‘Wakata miwa’ hao wa mkoani Kagera ili waweze kutisha msimu ujao.

Kagera ilinusurika kushuka daraja msimu uliopita baada ya kukamata nafasi ya 12 katika timu 16 zilizoshiriki baada ya kufanikiwa kukusanya alama 31 huku akikiri kutakiwa kufanya mabadiliko makubwa ndani ya kikosi hicho.

Adolf amesema anahitaji kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi hicho katika kila idara baada ya kugundua mapungufu mengi ambayo yaliwagharimu msimu uliopita.

“Tutafanya mabadiliko makubwa ndani ya kikosi, tutaongeza wachezaji katika kila idara ili tuweze kuleta ushindani wa kweli kwenye ligi msimu ujao, hatuwezi kuwa lonya lonya kama ligi iliyoisha” alisema Adolf.

Katika hatua nyingine kocha huyo alikataa kuwataja wachezaji atakao waacha msimu huu kabla ya kupata watakaoziba mapengo yao ili kuepuka kuzidiwa kete na timu nyingine.

“Muda ukifika tutawaweka hadharani kwa sasa tunafanya mawindo yetu taratibu ili kuimarisha kikosi chetu,” alisema Adolf.

Kuhusu kuingia kambini kujiandaa na mchakamchaka wa msimu ujao kocha huyo alisema muda si mrefu watatangaza utaratibu mzima wa mpango huo.

Afande sele: wasanii wengi watafta kiki siyo wabunifu
Giuseppe Marotta: Hatujapokea Ofa Yoyote