Kiungo wa klabu ya Sporting Lisbon pamoja na timu ya taifa ya Ureno Adrien Silva amethibitisha kuwa katika mipango ya kujiunga na mabingwa wa soka nchini England Leicester City.

Kiungo huyo ambaye alikua sehemu ya kikosi cha Ureno kilichotwaa ubingwa wa Euro 2016, amesema ataondoka Sporting kabla ya dirisha la usajili kufungwa kesho usiku.

Tayari imeripotiwa kuwa, Leicester City watamsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa ada ya pauni milioni 21.

Mpango huo wa Silva utakua unakamilisha ndoto zake kwenda kujiunga na  Islam Slimani ambaye walikua wote kwenye kikosi cha Sporting, na tayari mwezake ameshatangulia King Power Stadium.

“Baada ya miaka 15 ambayo nimekuwa na klabu ya Sporting, ninaamini nafasi hii ya kuondoka imekua kama bahati kwangu kutokana na hitaji langu la kutaka kubadilisha mazingira na changamoto ya soka langu.

“Ninaipenda Sporting kwa sababu nimeishi na wenzangu kama familia moja na nimekua hapa tangu nikiwa na umri wa miaka 12, hivyo ninajua ninachokizungumza kina maslahi gani kwangu na ni vipi nitakavyoendelea kupakumbuka hapa. Alisema Silva alipokua akihojiwa na gazeti la O Jogo la nchini Ureno.

Maafisa wauawa kwa silaha ya kutungua ndege Korea Kaskazini kwa amri ya Rais
Nacer Chadli Ailazimisha West Brom Kuvunja Benki