Tatizo la wanafunzi kuibia mitihani lipo karibu ulimwenguni kote. Hii hutokana na wanafunzi kutokusoma kipindi cha mitihani hivyo kuamua kujihami kwa kutengeneza majibu wakati mwingine kununua majibu kama jinsi ambavyo kesi nyingi zinavyojitokeza.

Tanzania wanafunzi wengi wameonekana katika mitihani ya kitaifa kuchora picha za wachezaji katuni au kufanya vile waonavyo kwa wakati huo baada ya kushindwa kupata jibu sahihi la swali katika mtihani huku kukiwa hakuna hatua za kisheria zinazochukuliwa, tofauti na hali iliyotokea huko India.

Mwanafunzi mmoja wa India amehukumiwa kifungo jela kwa kudanganya katika mtihani baada ya kujaribiwa kwa mara ya pili.

Ruby Rai mwenye umri wa miaka 17 ambaye alikuwa wa kwanza katika mtihani huo katika jimbo la Bihar, alisema katika mahojiano kwamba somo alipendelo la sayansi ya siasa linahusu mapishi.

Baada ya kanda hiyo kusambaa ,Bi Rai alilazimika kukaa tena mtihani na alikamatwa aliposhindwa huku matokeo yake ya mtihani yakifutiliwa mbali.

Aliwasilishwa mahakamani siku ya Jumapili ambapo hakimu alimuhukumu kifungo jela hadi tarehe 8 mwezi Julai.

Uamuzi wa kumpeleka jela umekosolewa kwa kuwa ni mtoto na kwamba badala yake angepelekwa katika jela ya watoto.

Gazeti la Hindu lilimnukuu Afisa Mkuu wa Polisi Manu Maharaj akisema kuwa Bi. Rai atalazimika kubaini kwamba yeye ni mtoto.

Wakati huohuo agizo la kukamtwa limetolewa kwa wanafunzi wengine ambao walifanya vyema katika mtihani akiwemo Sauragh Shrestha ambaye alikuwa wa kwanza katika somo la sayansi lakini ambaye baadaye alishindwa kusema kwamba H20 ni maji.

Video: Airtel FURSA Yatoa Msaada Kwa Vituo Vya Yatima Dar
Zijue Silaha za Kulinda Maahusiano Yako