Mwanaume mmoja raia wa Japan amepoteza maisha ndani ya ndege baada ya kumeza kete 246 za Cocaine akitokea mji wa Mexico.

Ndege hiyo iliyokuwa inaelekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Narita nchini Japan ililazimika kutua kwa dharula katika jimbo la Sonora nchini Mexico baada ya mwanaume huyo kupoteza fahamu.

Aidha mamlaka zimesema kuwa mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Udo N, alipoteza maisha baada ya ubongo wake kujaa maji kutokana na matumizi ya madawa kupita kiasi.

Kwa mujibu wa taarifa ya mwanasheria mkuu wa jimbo la Sonora, amesema wakati wa uchunguzi, Kete zilizokua na urefu wa sentimita 2.5 na upana wa sentimita 1 zilikutwa tumboni na kwenye utumbo.

Hata hivyo abiria wengine 198 waliobaki waliendelea na safari baada ya kutua kwa dharura katika mji wa Hermosillo, mamlaka za Mexico zimesema zitaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Uganda: Wanaosaidia ombaomba kufungwa
Video: Mwanamke mwenye misuli zaidi duniani

Comments

comments