Uongozi wa chama cha soka cha Argentina (AFA) umethibitisha kushindwa kufikia lengo la kuvunja mkataba wa meneja wa mabingwa wa soka nchini England Manchester City Pep Guardiola, ambaye walimpa kipaumbele cha kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa hilo.

AFA wapo kwenye mchakato wa kumsaka mbadala wa kocha Jorge Sampaoli ambaye alilazimika kufungasha virago, baada ya kushindwa kufikia makubaliano na uongozi wa chama hicho, ambao ulimtaka ajitathmini kwa kufaya kazi kama kocha wa timu za vijana, kabla ya kurejea kwenye kikosi cha wakubwa cha Argentina.

Sampaoli alitakiwa kufanya hivyo, baada ya mipango yake kushindwa kuiwezesha Argentina kufanya vyema katika fainali za kombe la dunia zilizomalizika nchini Urusi mwezi Julai, na kuaondolewa katika hatua ya 16 bora kwa kufungwa na Ufaransa mabao manne kwa matatu.

Mwenyekiti wa AFA Claudio Tapia ameiambia televisheni ya TyC Sports: “Tulijipanga kuvunja mkataba wa Guardiola, lakini tumeona kuna changamoto kubwa ya kufanya hivyo, kutokana na kiwango kikubwa cha pesa kuhitajika kukamilisha mpango huo!

“Kwa sasa hatuwezi kufanya hivyo, hatuna pesa za kutosha kufikia lengo la kumuajiri meneja huyu, tutaangalia mpango wetu wa pili ambapo tunaamini tutafanikiwa kumpata kocha mpya ambaye atakua na vigezo vya kuiwezesha timu yetu kufanya vizuri.

“Tunatarajia mazuri yatakuja baada ya kufanya kazi ya kujadilina kwa kina, kuhusu nani anaetufaa katika mchakato huu, japo kuna baadhi ya majina yameshaorodheshwa kwenye orodha yetu.”

Hata hivyo baadhi ya vyombo vya habari vya Argentina vimeleza kuwa, huenda wanaopewa nafasi ya kushika wadhifa wa kocha wa Argentina wakawa wazawa ambao wanafanya vizuri katika ligi za barani Ulaya.

Majina yanayotajwa ni Diego Simeone wa Atletico Madrid na Mauricio Pochettino wa Tottenham, lakini alipoulizwa mwenyekiti kuhusu wawili hao alisema: “Jambo hili bado linaendelea kufanyiwa kazi na ni mapema mno kusema tunamjadili nani katika vikao vyetu vya ndani, baada ya kuthibitisha kushindwa kumpata Guardiola.”

“Japo tunajipanga kufanya mazungumzo na makocha wetu wazawa Simone, Marcelo Gallardo, Pochettino na wengine, lakini ningependa kuwataka mashabiki kuendelea kusubiri na mpango huu utakapokamilika watafahamishwa.”

Kwa sasa kikosi cha Argentina kimekabidhiwa kwa makocha wa timu za vijana za nchi hiyo Pablo Aimar na Lionel Scaloni ambao kwa pamoja watakuwa katika benchi wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Colombia utakaochezwa mwanzoni mwa mwezi ujao.

Ni kweli nina madeni kwani Chadema inawahusu nini- Kalanga
Mbunge aivimbia TAKUKURU