Katika hali isiyotarajiwa, mwanamke mmoja wa Pakistani amejikuta akifanya ‘fungate’ maarufu kwa lugha ya kigeni kama honeymoon peke yake bila mumewe, tukio linalopaswa kufanywa na wanandoa.

Mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la Huma Mobin alifunga ndoa miezi kadhaa iliyopita na mumewe, Arsalan Sever na wawiwili hao walipanga kwenda kufanya fungate lao nchini Ugiriki, wakiamini ni sehemu watakayokula raha zaidi.

Hata hivyo, hali haikuwa kama walivyopanga baada ya mume wa Huma kunyimwa kibali cha kuingia nchini Ugiriki (Visa), huku mwanamke akikubaliwa kuingia nchini humo.

Kwamuhibu wa mtandao wa BuzzFeed, mwanamke huyo alijikuta nchini Ugiriki peke yake akilia usiku kucha, lakini aliuambia mtandao huo kuwa mama mkwe alimtia moyo na kumtaka ale raha peke yake kadiri awezeka, “make the best of it.”

Picha na jumbe alizoweka mtandaoni mwanamke huyo zilisababisha kupata umaarufu mkubwa na kuzungumziwa na vyombo vikubwa vya habari kama BBC na CNN, hadi wawili hao walipokutana tena.

HoneyMoon wawili

 

Linah Aiombea Baraka Ndoa ya Ex Wake
Jerry Muro Anawa Mikono, ajiweka kando