Mwanaume mmoja anayefanya kazi ya muziki nchini India amefanyiwa upasuaji wa ubongo wakati akiendelea kupiga gitaa lake juu ya kitanda cha chumba cha upasuaji.

Abhishek Prasad, ambaye alikuwa mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na kisha kuhamia katika kazi ya muziki, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa uliotajwa kwa lugha ya kigeni kama ‘Musician’s dystonia’.

Kutokana na ugonjwa huo, vidole vyake vitatu vya mguu wa kushoto vilikuwa vikipandiana punde tu anapoanza kupiga gitaa na kumsabibishia maumivu.

Jopo la madaktari lilishauri Prasad kuendelea kupiga gitaa lake wakati wa zoezi la upasuaji ili kuwasaidia kuliona tatizo linalomsumbua kwa urahisi zaidi.

“Hili tatizo linamtokea pale anapojaribu kupiga kifaa cha muziki; na muda halisi wa kupata mrejesho ni muhimu kwetu ili tuweze kubaini eneo husika linasababisha tatizo hilo kwenye ubongo na tuweze kulitatua,” alisema Dk. Sanjiv C C, ambaye ni daktari bingwa kutoka Chuo Kikuu cha British Columbia.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Prasad alisema kuwa aliamua kukubaliana na ushauri wa jopo hilo la madaktari kupiga gitaa lake wakati wa zoezi hilo baada ya kufanya majadiliano ya kina na daktari bingwa wa upasuaji, Sharan Srinivasan.

Mtanzania akamatwa na dawa za kulevya India
Barakah afunguka sababu za kuitosa Rockstar4000, awavaa 'mashabiki' hawa