Mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina la Lightness Kivuyo mkaazi wa Unga Limited jijini Arusha, amefariki dunia akiwa anaombewa nyumbani kwa mtu mmoja anayejiita ‘Nabii Rajabu’.

Dada wa marehemu, Juliana Kivuyo amesema kuwa ndugu yake alikuwa anaumwa na alipelekwa na mumewe kwa ajili ya maombezi kwa Nabii Rajabu lakini alianguka na kufariki dunia wakati huduma ya maombezi ikiendelea.

“Baadaye shemeji alikuja nyumbani akihema, huku anadai kuwa dada alikuwa kwenye hali mbaya kule kwenye maombi,” Juliana anakaririwa na Habari Leo.

Anasema kuwa baada ya kufika katika eneo la tukio alimkuta ndugu yake akiwa amelazwa kwenye kochi akiwa bila nguo bali mwili wake umefunikwa na khanga na kwamba tayari alikuwa ameshakufa.

Kwa mujibu wa Mganga Mkuu katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, Jacqueline Uriwo, walipokea mwili wa Lighteness huku waliomleta wakijidai kuwa wamemleta mgonjwa na sio marehemu, lakini baada ya kumpima waligundua alikuwa amefariki muda mrefu uliopita.

Imeelezwa kuwa mume wa marehemu alisisitiza kuwa mke wake hajafa bali amezimia na kwamba huzimia kwa muda mrefu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Charles Mkumbo alithibitisha tukio hilo na kwamba watu wawili wanashikiliwa na jeshi hilo.

Koeman: Nilitamani Kumsajili Depay Nikiwa Southampton
Mwanafunzi wa UDOM kizimbani kwa kufadhili magaidi wa Al-shabaab