Mkazi wa Kijiji cha Rubambangwe Kata ya Muungano Wilayani Chato Mkoa wa Geita, Pascal Kanyembe (39) anadaiwa kufariki dunia akiwa mikononi mwa askari wa doria.

Kanyembe alifariki dunia saa sita mchana Julai 23, 2018 muda mfupi baada ya kufikishwa katika hospitali ya wilaya ya Chato kwa ajili ya matibabu baada ya kukamatwa akituhumiwa kujishughulisha na uvuvi haramu.

Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kukiri mtuhumiwa kupoteza maisha akiwa mikononi mwa vyombo vya ulinzi na kwamba jeshi la polisi linachunguza chanzo cha kifo hicho.

“Hakuna shaka marehemu alikuwa miongoni mwa watuhumiwa na alikuwa kwenye mikono halali na chini ya ulinzi halali, uchunguzi wa kidaktari umefanyika Julai 24,2018, taarifa kamili za nini kipo juu ya kifo cha marehemu zitatolewa baadaye,” amesema Mwabulambo.

 

Mohamed Salah amkuna Juergen Klopp
Video: Chadema waamsha kifo cha Akwilina, Waziri Lugola aibua ufisadi mpya NIDA

Comments

comments