Shabiki wa klabu ya mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC, Peter Kiliti ameripotiwa kufariki dunia wakati akishangilia ushindi uliyopata timu yake dhidi ya AS Vita Club.

Kupitia akaunti yao ya kijamii ya Instagram, Simba imetoa habari hiyo kwa kupoteza mmoja kati ya mashabiki wake ambaye amefariki dunia.

”Tumepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha shabiki wetu, Ndg Peter Kiliti ambacho kimetokea Wilaya ya Mpanda, Katavi wakati akishangilia ushindi tuliyoupata dhidi ya AS Vita ambao umetuwezesha kufuzu kucheza hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika,” imesema Simba SC.

Simba SC imeongeza ”Uongozi unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na watu wote ambao wameguswa na msiba huu. Pumzika kwa amani Mwanasimba mwenzetu”.

Simba SC ilikuwa na kibarua kizito siku ya Jumamosi dhidi ya AS Vita kwenye mchezo wa mwisho wa ligi ya Mabingwa Afrika ambapo ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2 – 1 uliyowawezesha kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, hii ni baada ya kupita miaka mingi.

 

Spika Ndugai amvutia pumzi mbunge mwingine Chadema
Katibu Mkuu Chadema ampongeza Maalim Seif

Comments

comments