Mwanamke mmoja barani Ulaya afariki dunia baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuongeza makalio, mwanamke huyo aliamua kufanya upasuaji wa bei nafuu unao julikana kama “Brazillian butt lift” (BBL) upasuaji huo unafanyika kwa kutoa mafuta sehemu ya mwili na kupachika katika makalio kwa muhitaji.

Wataalamu wa afya nchini Uingereza wameonya kuwa upasuaji huo ni hatari zaidi kuufanya lakini wanawake wengi  huamua kuufanya kwa kuongeza makalio kwani una bei nafuu zaidi ukilinganisha na upasuaji wa aina nyingine.

Pia wameongeza kuwa ongezeko la wanawake wanaopata matatizo kutokana na kufanya upasuaji wa kuongeza makalio lina endelea kwa kasi kwani kuna hatari ya kuweka mafuta ya mwili katika mishipa mikubwa ya makalio inayo safari hadi kwenye moyo na akili.

Upasuaji wa kuongeza makalio  kwa wanawake barani Ulaya na ulimwenguni kote umekuwa maarufu baada ya watu maarufu wengi kufanya na kufanikiwa na anaye wavutia sana kufanya upasuaji huo ni mwanamitindo maarufu kim Kardashian na msanii wa muziki Nick Minaj.

Naby Keita yupo 'FIT', kurudi Anfield leo
Haji Manara ajibu tuhuma za utovu wa nidhamu

Comments

comments