Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa 72) imeipa Arusha FC ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya African Sports kuchezesha wachezaji wawili waliotumia leseni za kughushi (non qualified) katika mechi ya Kundi B Ligi Daraja la Pili (SDL) kati ya timu hizo iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

 

Uamuzi huo dhidi ya African Sports umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(17) na 42(23) za Ligi Daraja la Pili. Nayo Arusha FC imepewa ushindi kwa kuzingatia Kanuni ya 14(36) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Taratibu za Mchezo. 

 

Vilevile viongozi wa African Sports waliohusika kughushi leseni zilizotumiwa na wachezaji hao ambao hawakusajiliwa watafikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya TFF kwa ajili ya hatua zaidi.

95 wapoteza maisha kwa kimbunga cha vumbi
Rufaa ya Young Africans yawekwa kapuni