Mtoto wa miaka sita (jina lake linahifadhiwa) katika Kata ya Nyombo, Manispaa ya Njombe amebainika kuingiliwa kimwili na kuharibiwa sehemu zake za siri na mtu aliyetajwa kuwa ni baba yake mdogo.

Akizungumzia wa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issa amesema kuwa mtoto huyo ambaye huishi na bibi yake, majira ya jioni bibi huyo hutoka kwenda kwenye vilabu vya pombe kujiburudisha na kurejea nyumbani usiku.

Ambapo muda huo baba mdogo anautumia muda huo kama nafasi ya ya kumwingia mtoto huyo na kumfanyia ukatiri wa kingono mara kwa mara.

Kamanda Issa amesema kuwa baada Jeshi la Polisi kupewa taaarifa uchunguzi ulifanyika na kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo, halikadhalika uchunguzi wa madaktari nao ulithibitisha kuwa ni kweli binti huyo alikuwa akiingiliwa kimwili na ameharibiwa sehemu zake za siri.

hata hivyo Mpaka sasa mtuhumiwa huyo amefikishwa Mahakamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Wizara ya Afya, NTLP, KNVC yaja na mpango wa kupunguza TB
Waitara awaonya wadai rushwa za ajira