Jeshi la Polisi Mkoani Katavi, linamshikilia Afisa mipango miji wa Halmashauri ya Mpimbwe Mkoani Katavi, Dickson Mwenda (37), kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka 15 kwenye gari lake.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mbele ya Waandishi wa Habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ali Makame Hamadi amesema tukio hilo limetokea Agosti 13, 2022 majira ya jioni katika Kijiji Kibaoni kilichopo Mkoani humo.

Amesema, siku ya tukio mama mzazi wa binti muathiriwa akiwa na mtuhumiwa baada ya kuwa pamoja kwa vinywaji alimkabidhi mtoto huyo na mdogo wake ili awapeleke nyumbani lakini wakiwa njiani mtuhumiwa aliegesha pembeni ya barabarana kisha akatekeleza tukio hilo ndani ya gari lake.

Kamanda Makame amesema, mtuhumiwa huyo aliyetumia gari lake aina ya Toyota lenye namba za usajili T 927 DMC, tayari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mlele kujibu tuhuma zinazomkabili.

Taifa Stars mguu sawa kuikabili Uganda
Singida Big Stars yachimba mkwara mzito Ligi Kuu