Afisa wa Polisi Mkoani Arusha aliyetajwa kama PC Halfani, alikutwa akiwa amejinyonga katika eneo la kambi ya makazi ya askari wa jeshi la polisi jijini humo jumapili iliyopita.

Askari huyo ambaye alikuwa anahusika na ulinzi wa kutumia polisi na farasi alikutwa na wakazi wa eneo hilo akiwa amening’inia juu ya mti huku sababu za kujitoa roho kwa hali ya kusikitisha zikiwa kitendawili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo japo alikataa kutoa maelezo kuhusu tukio hilo akidai kuwa hilo ni tukio lisilopaswa kutolewa maelezo kwa umma.

“Mambo yanayohusiana na polisi hayapaswi kwenda kwenye vyombo vya habari,” alisema Liberatus Sabas.

Wakazi wa eneo hilo la makazi ya polisi walitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu kabla haujasafirishwa kwenda mkoani Singida kwa ajili ya mazishi.

 

 

 

Rais Magufuli, Dk. Slaa Walikubaliana Katika Hili
TRA Yafafanua Kuhusu Watumishi Wake Kutangaza Mali Zao