Jeshi la Polisi mjini Memphis la kusini mwa nchi ya Marekani Tennessee, limewachukulia hatua za kinidhamu Polisi sita kwa kushiriki kumpiga na kumsababishia kifo Tyre Nichols.

Ofisa wa Jeshi hilo, Preston Hemphill naye amefutwa kazi licha ya kuwa bado hajafunguliwa mashtakata kwa makosa yoyote na Polisi hawajaweka wazi ushiriki wa polisi huyo katika tukio la kumkamata na kumpiga Nichols.

Afisa wa Polisi, aliye achishwa kazi, Preston Hemphill. Picha ya Reuters.

Maafisa wengine watano wamefunguliwa mashatika kwa mauaji ya kiwango cha pili, kupiga, kuteka, kutowajibika na ukandamizaji wakiwa kazini.

Maafisa hao watano ambao walifutwa kazi wote ni weusi na Polisi ilitoa picha za video zikionyesha Polisi hao wakimpiga vibaya Nichols mapema mwezi huu baada ya kumsimamisha barabarani.

George Weah atangaza kugombea tena Urais
Sadio Mane akiwasha The Bavarians