Baada ya kufanikiwa kupanda daraja mwishoni mwa majuma mawili yaliyopita wakitokea ligi daraja la kwanza hadi ligi  kuu ya soka Tanzania bara, msimu ujao wa mwaka 2016-17, klabu ya soka ya Africa Lyon imejinasibu kuleta upinznai mkali dhidi ya klabu za ligi kuu.

Kocha msaidizi wa Afrika Lyion Renatus Bernard amesema timu yake inajipanga kwa sasa kwa ajili ya ligi hiyo ikiwa ni pamoja na kujaribu kuongeza wachezaji wenye uzoefu wa kupambana.

Benard amesema wanasubiri dirisha la usajili litakapofunguliwa mwishoni mwa msimu huu, ili waanza mpango wa kuwasajili wachezajia mbao watawaona wanafaa kwa ajili ya msimu ujao wa ligi, japo hakutaka kueleza kwa kina ni wapi walipoelekeza nguvu zao katika usajili.

African Lyon walipata nafasi ya kurejea kwenye ligi kuu ya soka Tanzania bara, baada ya kulazimisha matokeo ya sare ya bao moja kwa moja dhidio ya Ashanti Utd, katika mchezo wa kundi A.

Azam FC v Prisons, Hall Atamba Kurejea Kileleni Kesho
Kazimoto Aomba Msaada Wa Wakili