Bara la Afrika limethibitisha kumuunga mkono rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino, kuelekea uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo utakaofanyika mapema mwaka 2019.

Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad amesema wataendelea kumuunga mkono kiongozi huyo ambaye aliingia madarakani miaka miwili iliyopita, katika uchuaguzi mdogo uliofanyika baada ya kuondolewa kwa aliyekua rais wa FIFA, Sepp Blatter, kufuatia sakata la rushwa.

Ahmad alithibitisha mpango wa kuungwa mkono kwa Infantino, baada ya mkutano mkuu wa CAF uliofanyika jana Jumapili nchini Misri.

“Sio Afrika pakee inayomuunga mkono Infantino, tupo wengi tuliodhamiria kumchagua tena kiongozi huyu katika uchuguzi mkuu ujao, tuna imani naye kubwa katika maendeleo ya soka duniani,” alisema Ahamd.

“Tutakwenda kwenye uchaguzi mkuu tukiwa na dhamira moja ya kumchagua ili aendelee kuliongoza soka la dunia nzima, kwa hakika tangu alipoingia madarakani tumeona namna anavyoujali mchezo huu, na kulitazama bara la Afrika kwa jicho la tatu, ili kufanikisha maendeleo ya mchezo huu pendwa barani kwetu,” aliongeza.

Hata hivyo, wakati CAF wakitangaza kumuunga mkono Infantino kuelekea uchaguzi mkuu wa FIFA, bado wadau wengine wa soka duniani hawajatangaza nia ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya urais wa shirikisho hilo.

Video: Aika amuweka wazi aliyemuandikia ‘Katika’
Lugola ashusha rungu polisi, ''Marufuku kushindwa kutoa dhamana''