Leo Wanachama wa Shirika la Afrika Diaspora Forum wameandamana Afrika Kusini kushinikiza serikali ya nchi hiyo na Tanzania kubaini ukweli kuhusu kuuawa kwa mwanafunzi raia wa Tanzania, Baraka Leonard Nafari.

Hatua hiyo ni kufuatia na namna ambavyo mwanafunzi huyo aliuawa ambapo kutokana na video iliyoonekana kupitia kamera za CCTV zilizopo chuoni hapo zimeonesha dereva huyo wa teksi  akimgonga kwa makusudi mwanafunzi huyo kwenye uzio wa makazi ya chuo yaliyoko Auckland Park.

Moja ya mwanachama wa Africa Diaspora Forum, Marc Gbaffou ametaka tukio hilo la kuuawa kwa Baraka liwekwe wazi na lifanyiwe kazi.

Maafisa wa shirika hilo pia wameandamana kwa pamoja na baadhi ya wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Johannesburg nje ya bweni linaloitwa Sophiatown ambapo mwanafunzi huyo aligongwa na kufariki.

Maandamano hayo yalikuwa salama na watu walikusanyika kwenye uzio mahali gari lilipo mgonga marehemu Baraka Naferi wakiwa wamebeba mabango yanayosema tunataka haki kwa Baraka, haki itendeke kwa Baraka.

Hata hivyo mtuhumiwa alikamatwa na polisi wa Afrika Kusini lakini baadaye akaachiliwa huru kwa dhamana. Polisi walisema hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa kumfungulia mashtaka ya mauaji.

Baraka Nafari alikuwa akichukua Shahada ya Uzamivu (PHD) katika Chuo Kikuu cha Johannesburg (UJ) aliuawa kikatili Ijumaa Februari 23, mwaka huu.

Wachungaji 6 waswekwa ndani
Wanawake waandamana kuomba Rais adhibiti ulevi wa wanaume