Nchi ya Afrika Kusini imeendelea kuomboleza kifo cha mke wa zamani wa rais wa kwanza Mweusi wa nchi hiyo, Nelson Madiba Mandela, na mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi, Winnie Mandela aliyefariki jana Jumatatu Aprili 2, 2018.

Serikali ya Afrika Kusini imetangaza kwamba itaandaa matukio kadhaa kuelekea mazishi ya  Winnie Mandela aliyejitoa muhanga kupiga vita utawala wa ubaguzi wa rangi.

Winnie Mandela alifariki jana Jumatatu katika hospitali ya Johannesburg akiwa na umri wa miaka 81 baada ya kuumwa kwa muda mrefu.

Wafuasi na wananchi wa Afrika kusini tangu kutangazwa kwa kifo chake wamekukusanyika mbele ya nyumba yake iliopo mji wa Soweto huku wakiimba nyimbo za harakati walizokua wakiimba wakati wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Kwa upande mwingine Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, kiongozi wa chama tawala cha African National Congress (ANC), amesema Afrika Kusini inaomboleza kifo cha mwanamama huyo na serikali itashirikiana na familia wakati wa mazishi yake rasmi yatakayofanyika Aprili 14.

Juma Nature, Marlow, Mandojo wamuumiza kichwa Ray C
Mbowe atoa neno baada ya kuachiwa huru, adai kufichua mazito