Mwanaume mmoja nchini Kenya amehukumiwa kifungo chamiaka mitatu jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua na kumchuna ngozi paka.

Mahakama Mjini Nakuru ilifikia uamuzi huo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo ulioonesha kuwa James Kimani alikutwa akiwa anamchuna paka ngozi kwa ajili ya kuuza nyama yake.

Kesi hiyo ilikuwa miongoni mwa kesi maarufu mjini humo baada ya gazeti la Daily Nation kuripoti namna ambavyo mtu huyo alikamatwa na kushambuliwa na watu wenye hasira kali.

Kimani alidai kuwa amekuwa akifanya biashara ya kuuza nyamaya paka kwa miaka saba na kwamba alikuwa anawauzia watu ambao walikuwa wanafanya biashara hiyo.

Mahakama ilieleza kuwa Sheri ya Udhibiti wa Nyama nchini humo haiitambui nyama ya paka kama nyama inayopaswa kuliwa na binadamu.

Hata hivyo, ingawa nyama ya paka inachukuliwa kuwa mwiko nchini Kenya, ni chakula kitamu kwa baadhi ya nchi za Afrika Magharibi.

Paka huliwa pia nchini China, Vietnam na Korea. Katika nchi hizo, nyama ya paka huliwa ikiwa yenyewe au kwa kuchanganywa na nyama nyingine ili kuongeza ladha.

Ripoti zataja nchi hatari zaidi kwa wanawake kuishi
Wizara ya Afya yatoa tahadhari ugonjwa wa Dengue, Chikungunya