Mkazi wa Mbagala, wilayani Temeke Jijini Dar es Salaam, Mwanatoli Huruma Mjumbe mwenye umri wa miaka 54 amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumlawiti mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 11.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumanne Desemba 15, 2020 na hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya Wilaya ya Temeke, Karim Mushi akibainisha kuwa mshtakiwa huyo alikuwa anakabiliwa na mashtaka mawili ya kumbaka na kumwingilia mwanae kinyume na maumbile.

Mushi amesema kati ya Januari 2017 na Februari 19, 2019 maeneo ya Mbagala, mshtakiwa huyo alimbaka na kumwingilia kinyume na maumbile mtoto huyo.

Amesema ushahidi uliotolewa na mtoto huyo haukuwa na shaka kwa kuwa mshtakiwa huyo alipokuwa akirudi nyumbani kwake usiku alikuwa anamlazimisha kwenda naye chumbani kwake na kuanza kumwingilia.

Ametoa hukumu hiyo akisisitiza kuwa lengo ni kuwa fundisho kwa wengine wenye tabia kama ya mshtakiwa huyo.

ACT wakubali yaishe, wabunge wala kiapo
Dkt. Mwinyi avunja bodi ya Wakurugenzi