Mwanamuziki Selena Gomez ameungana na Rais Biden na utawala wake kuweka uangalizi juu ya masuala yanayohusu afya ya akili.

Gomez na utawala wa Biden wameamua hayo ili kuangazia namna ya kuwa msaada kwa kundi kubwa la vijana ambao wamekuwa wakikabiliwa na tatizo hilo linaloendelea kushamiri kwa kasi kote duniani.

Mwimbaji huyo mahiri jumatano ya wiki hii alihudhuria’1600 Pennsylvania Ave’ katika Ikulu ya Marekani, kutoa hotuba na kusaidia kuongoza mazungumzo na Jukwaa jipya la hatua, linaloshughulikia vijana wanaokabiliwa na tatizo la afya ya Akili, ambalo lilisimamiwa na MTV pamoja na Rare Beauty’s Rare Impact Fund.

Selena alitambulishwa na mke wa Rais wa Marekani Dk. Jill Biden, na kisha akaweka wazi sababu za yeye kushawishika na kujiunga na kampeni hiyo na kwa nini ni muhimu kuwawezesha watu kujadili juu ya masuala ya kuhusu tatizo la afya ya akili kwa uwazi zaidi.

Alidokeza mambo kadhaa ikiwamo kufafanua dhamira ya wazo na umuhimu wa kuendelea kwa kampeni hizo kuwa ni kukomesha unyanyapaa kwa wenye tatizo la afya ya akili, kuwainua viongozi vijana wanaofanya kazi katika nyanja hiyo, utetezi, ujasiriamali nk.

Bila shaka kwa wenye kufuatilia mwenendo wa maisha ya nyota huyo watakuwa wanafahamu ambavyo, aliwahi kuweka hadharani baadhi ya changamoto zake za afya ya akili, licha ya kuwa kwa sasa amerejea katika hali yake kawaida.

Muna Love adhihirisha uchungu wa kuzushiwa kifo
Wanaosambaza taarifa za uongo Chanjo ya Polio kupambana na Usalama