Muigizaji maarufu wa filamu za mapigano ya mitindo ya Kung-fu na Tai-Chi, Jet Li yuko katika hali inayohitaji msaada wa kiafya, inayomsababisha kuonekana kama mzee mwenye umri mkubwa tofauti na umri wake.

Jet Li mwenye umri wa miaka 55 ambaye mwaka 2013 aliweka wazi kuwa anasumbuliwa na ugonjwa unaofahamika kitaalam kama ‘hyperthyroidism’ alionekana hivi karibuni na kupiga picha na shabiki mmoja, picha inayoonesha ugumu kumtambua.

Muigizaji huyo alieleza kuwa ana tatizo la majeraha kwenye uti wa mgogo yanayosababisha ashindwe kusimama kwa muda mrefu bila kuinama au kugemea kitu.

Kijana aliyeonekana akiwa kwenye picha ya pamoja, aliliambia gazeti la South China Morning Post kuwa alipomuona alishindwa kumtambua kwa haraka na kwamba alikuwa anatembea kama mtu anayehitaji msaada.

Jet Li (kushoto) katika tuzo za mwaka 2008

“Alikuwa amechangamka kabla lakini sasa hivi anaonekana kama mtu mzee sana,” alisema kijana huyo.

Hivi karibuni, Jet Li amejikita maisha yake katika kazi za kujitolea kusaidia watu wenye mahitaji maalum. Pia, alisema kuwa imani yake ya Ki-Buddha pamoja na kusoma vitabu vya dini kumemsaidia zaidi kupata nafuu.

Jet Li amefanya filamu nyingi na kubwa za mapigano ikiwa ni pamoja na Tai Chi, Shaolin Temple, Romeo Must Die, Fearless, The One, The Shaolin Temple, The Expendables, Fist of Legend, Cradle to the Grave na nyingine nyingi.

WCB kuandaa tamasha kubwa nchini ''Wasafi Festival''
Heche aitaka serikali kuacha kuwatesa wafugaji