Uongozi wa timu ya KMC umewataka mashabiki wao wasiwe na hofu na mlinda mlango wao namba moja Juma Kaseja ambaye amefanyiwa upasuaji wa goti hivi karibuni.

Ofisa Habari wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa kwa sasa maendeleo ya Kaseja yanaridhisha hivyo mashabiki wasiwe na wasiwasi.

“Kwa sasa maendeleo ya Kaseja sio mabaya kwani ameanza kurejea kwenye ubora wake taratibu kabla ya kuungana na wachezaji wenzake kuendelea na majukumu yake ya kila siku.

“Muda rasmi ambao atakaa nje kwa sasa bado ni ngumu kutambua kwa kuwa ripoti ya daktari hatujaipokea na bado yupo kwenye uangalizi ili awe imara zaidi tunatarajia hatakaa nje kwa muda mrefu,” amesema Binde.

Kaseja aliyejiunga na KMC msimu wa mwaka 2018-19 ilipokuwa chini ya Etienne Ndayiragije kutoka Kagera Sugar aliukosa mchezo dhidi ya Simba ambao KMC walipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 uwanja wa Uhuru kutokana na kuwa majeruhi.

Kocha Simba: bado naangalia viwango vya wachezaji wangu
Kigwangalla, Katibu mkuu wake kitanzini siku 5, Mwaka 2019 ulikuwa ni mwaka wa 'vyuma kukaza'