Waziri wa Fedha na Mipango, Tanzania Philip Mpango leo Februari 23, 2021 ameruhusiwa kutoka katika hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma Waziri Mpango amewahakikishia wanachi kuimarika kwa afya yake na kurudi kulitumikia Taifa.

Aidha, Mpango amemshukuru Mungu kwa huruma yake kwa kumfikisha hapo alipofikia na kwa afya yake kuimarika ambapo pia amemshukuru Rais John Magufuli na familia yake kwa ujumla na viongozi wa wote wa Serikali na dini kwa maombi yao juu yake.

Waziri Mpango amewashukuru wananchi wa jimbo lake la Buhigwe na kuwasihi wasiwe na wasiwasi wakae na amani huku akibainisha kuwa muda si mrefu atarudi kuwatumikia.

Ameendelea kuwashukuru wahudumu wa afya wote waliomtibu kwa wakati wote toka alipoanza kuugulia nyumbani na kufikishwa hospitalini

Sambamba na hayo Waziri Mpango ametoa pole kwa wanafamilia waliondokewa na wapendwa wao ikiwemo familia ya Maalim Seif Sharif Hamad, familia ya Balozi Kijazi, familia ya Atashasta Nditiye na familia ya Profesa Benno Ndullu.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Februari 24, 2021
TP Mazembe kulipa kisasi kwa Al Hilal?